KILIMO CHA PAMBA

Msemaji wa serikali kanali Cyrus Oguna amewataka vijana kuegemea kilimo ndipo waweze kujiajiri na kuwacha kutegemea kazi za kuajiriwa.

Akizungumza kwenye kiwanda cha Rivatex Eldoret alidokeza kuwa vijana wengi wanategemea kuajiriwa na wana uwezo wa kujiinua kimaisha  kutokana na kilimo cha aina yoyote  hasa upanzi wa pamba akisema kuwa soko iko tayari.

Oguna amewahimizi vijana kuwacha dhana kuwa kilimo haina manufaa akiwasuta kuwa watu wa kujikakamua kimaisha ndipo maisha yao ya hapo baadae iweze kuwa ya matumaini.

Wakati huo,meneja wa kiwanda hicho Patrick Nyaga amedokeza kuwa tayari kiwanda hicho imeweka mikakati ya kutosha ya kuwapa miche na mbegu ya pamba kwa vijana hao waweze kuendeleza kilimo hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *