Viongozi wa dini la kiislamu kaskazini mwa bonde la Ufa wameendelea kutoa wito kwa wakenya kuhakikisha wanalinda mali na maisha ya wengine wanapoingia kwenye maandamano ili kupunguza visa vya maafa yanayoshuhudiwa wakati wa zoezi hilo.
Wakiongozwa na mwenyekiti wa baraza la maimamu ukanda huo Sheikh Abubabakar Bini ni kwamba licha ya kuwa maafisa wa usalama wakati wa maandamano ya Saba Saba kujizuia na kuhakikisha kila mwandamanaji anapata usalama wa kutosha,wanaoanamdana ndio wameonyesha nia ya kupora na kuwashambulia wengine.
Kulingana naye,taifa haliwezi jengwa kwa chuki na kisasi bali kwa uwiano na mazungumzo kwa suluhu la kudumu.
