Papa Leo atoa wito wa amani Mashariki ya kati

Baba mtakatifu Leo wa kumi na nne amesema mgogoro wa Mashariki ya Kati umefikia katika kiwango kibaya sana, na amezihimiza pande zinazohusika kuheshimu sheria za kimataifa.

Papa Leo, ametoa tamko hilo mjini Vatican alipokutana na maaskofu na viongozi wa mashirika ya misaada kutoka eneo la Mashariki ya Kati.

Akionekana kutumia lugha yenye mchanganyiko wa mafumbo katika kikao hicho, Papa Leo amesema kwamba mataifa ya ukanda huo yameathiriwa vikali na vita vya mara kwa mara, vinavyosababisha mataifa hayo kupokonywa haki zao za msingi, kwa maslahi ya kisiasa huku eneo zima likiendelea kufunikwa na wingu zito la chuki ambalo limechafua hata hewa wanayovuta.

Akionekana kusikitishwa na kile kinachoendelea kutokea katika eneo la mashariki hasa Gaza, Papa Leo ameomba uwepo wa Mungu kwa kuwapa masikio ya kiroho wale wenye kuhusika na utatuzi wa mzozo huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *