SHA imekuwa chungu kwa watoto Elgeiyo Marakwet

Idadi kubwa ya watoto katika kaunti ya Elgeyo Marakwet wanakosa huduma muhimu za afya kutokana na kutosajiliwa kwenye bima mpya ya afya maarufu kama SHA.
Haya ni kwa mujibu wa afisaa mkuu anayesimamia maswala ya afya katika kaunti hiyo Caroline Magut, akizungumza na wanahabari ofisini mwake mjini Iten, afisaa huyo amedokeza kuwa, wazazi wengi hawajesajili wanao chini ya mpango huo huku akiwarai wakazi katika kaunti hiyo kuhakikisha kuwa wamesajili wanao chini ya mpango huo.
kwa sasa asilimia 52.6% ya wakazi katika kaunti ya Elgeyo Marakwet wamejisali kwenye mpango huo idadi kubwa ikiwa ni watu wakubwa pekee .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *