Vijana wametakiwa kuwa watiifu na wenye nidhamu kwa faida ya siku zao za baadaye kuwa kuwa kizazi cha sasa almaarufu kinaonekana kupoteza maadili kwa kiwango cha juu.
Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nyeri Anthony Muheria amewataka vijana kuwa na subira na watiifu akihoji kuwa ilivyo kwa sasa nay ale yaliyoshuhudiwa kwenye maandamano ya siku ya jumatano iliyopita ni ukosefu wa nidhamu na kupotea kwa maadili miongoni mwao Jamabo analosema kuwa huenda ikawaathiri katika siku zao za baadaye.
Askofu Muheria kadhalika ametoa wito kwa viongozi kutoka pande za serikali na upinzani kulegeza matakwa yao na kamwe kutochochea vijana akisema kuwa uchochezi huo huenda ikazamisha taifa hili katika lindi la machafuko akitoa wito kwa kila upande kukubali maridhianao kwa lengo la mshikamano wa kitaifa
