Viongozi wa kisiasa katika kaunti ya Uasin Gishu wanaendelea kujitokeza na kuwanyoshea kidole cha lawama kwa upinzani kwa kile wanasema kukosa mwelekeo kwenye siasa zao.
Wa hivi punde ni naibu gavana wa kaunti hiyo Evans Kapkea ambaye amewataka wapinzani kukoma kueneza siasa za kumsuta rais Ruto kwa kuimba neno One Term kwani anasema wanaamini Rais ni mchapakazi na atarejeshwa pindi uchaguzi mkuu utakapowadia.
Amesisitiza haja ya wakenya kumuunga mkono rais kwa kuwa malengo yake ni kwa wote huku akiwataka wapinzani kutafuta njia mbadala ya kujiimarisha kisiasa na kukoma kumhusisha rais na siasa zao ambazo anasema hazina mwelekeo.
