Taifa likionekana kukosa maelewano baina yake na wananchi,wito umetolewa kwa uwaiano na mshikamano miongoni mwa wakenya kupitia kwa ujamaa wema.
Askofu wa jimbo katoliki la Embu Peter Kimani Ngungu’ amesikitikia kile anasema kukosekana kwa Amani nchini kutokana na matukio ambayo yameshuhudiwa nchini kufuatia maandamano ambayo kikatiba yanafaa kuwa ya Amani licha ya wanaoandamana siku za hivi majuzi kuonekana kushiriki maswala yasiyofaa kama vile uporaji na kuwaua kwao.
Askofu Kimani vilevile,amewataka vijana nao kuwa wenye subra na kukumbatia swala la mazungumzo kwa manufaa ya kuwepo kwa maelewano nchini,huku akieleza kwamba mashindano baina ya serikali na vijana haiwezi fanikisha uchumi wala Amani nchini.
Aidha,askofu huyo amesisitizahaja ya vijana kujitenga na viongozi au mkenya yeyyote ambaye atawaadaa kuzua vurugu nchini akieleza kuwa taifa hili lawategemea wao siku za halafu na pindi wanashiriki mchezo wa kuvuruga na kuahribu taia,hawatakuwa na lolote la kujenga hapo baadaye.
