B.KIMENGICH:Acheni kupimana nguvu Nchi ni moja tu!

Taifa likionekana kuwa katika hali ya mshikemshike kutokana na visa vya mauaji na kutumia nguvu kupita kiasi kutoka kwa maafisa wa usalama wanapokabili umma yanayaoandmaana,askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich ametaka umma kuwa makini na namna wanavyochukua sheria isije ikaingiza taifa pabaya.

Askofu Kimengich alisikitia swala hilo akitaja kama swala lisipodhibitiwa hivi karibuni,taifa litatumbukia katika njia isiyokuwa salama.

Kiongozi huyo wa kidini anataka haki pia itendeke kwa waathiriwa na maafisa wa usalama kuhakikisha wanazingatia sheria huku akiwataka wananchi nao kuwaheshimu maafisa wanapotumwa kuwalinda.

Askofu aidha,aliwaomba wenyeji katika bonde la Kerio kuwazia upya uhusiano wao na majirani zao ndipo suluhu la kudumu liweze kupatikana kutokana utovu wa usalama ambao umewanyima wananchi wengi Amani hata wengine kupoteza maisha yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *