Tuachieni Nyakango’ ni huyo tu

wawakilishi wadi katika kaunti ya Uasin Gishu wameghadhabishwa na jinsi baraza la magavana kupitia kwa mwenyekiti wake Adhulahi Ahmed kwa kutaka kumngatua afisini Controller wa Bajeti Margaret Nyakango’ kwa kile wanasema kutumia afisi vibaya.

wawakilishi hao wakiongozwa na mca wa Langas Francis Muya na mwenzake wa Kapseret wamesema kwamba Nyakango’ amefanya kila awezalo kuhakikisha kwamba pesa za mkenya zinalindwa na iwapo watachukua mkondo huo,mkenya wa kawaida hawezi kupata haki kwa matumizi ya serikali na ataendelea kuumia akitozwa ushuru kila kuchao.

sasa wawakilishi hao wanamtaka rais William Ruto kuingilia kati na kuweka sawa mambo ndipo taifa lisije likatumbukia pabaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *