Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nyeri Anthony Muheria ametoa wito kwa jamii kujitolea kuwasaidia watoto wanaougua ugonjwa wa tawahudi yaani Autism katika jamii.
Akizungumza baada ya kuzindua kituo cha kuwasaidia watoto walio na ugonjwa wa tawahudi bila malipo jimboni humo askofu mkuu Muheria amesema kuwa watoto hao wanahitaji kushughulikiwa kwa umakini zaidi akitoa wito kwa jamii kadhalika kuwasaidia wazazi wa watoto hao ikizingatiwa kuwa wengi wao hupatwa na unyanyapaa.
Amesema kuwa hii itakuwa afueni kwa wakaazi hao kwa kuwa hospitali hiyo sasa itatoa huduma nyingi ya kukabiliana na ugonjwa huo bila malipo, badala ya kiasi kikubwa cha fedha zinazotozwa kwa wagonjwa wanaougua maradhi hayo.
Nao wazazi wa watoto wanaougua maradhi hayo wameonyesha furaha yao baada ya kupata huduma katika hospitali hiyo.
