Hatimaye Padre Allois Cheruiyot Bett amezikwa hii leo katika makaburi ya Parokia ya Ol’lessos kaunti ya Nandi.
Maelfu ya waombolezaji wakiwemo, maaskofu, mapadre, watawa, wakristu na viongozi wa tabaka mbalimbali, walikusanyika katika uwanja shule ya upili ya wavulana ya Terige kwa Misa ya mazishi na kutoa heshima zao za mwisho kwa mwendazake.
Katika homilia yake, askofu msaidizi wa jimbo Katoliki la Eldoret John Lelei amemtaja padre Alloys kama aliyejitolea katika utume wake na kwamba kifo chake kimelipokonya jimbo zima mchungaji mwema na wote waliomuenzi.
Wakati uo huo askofu Lelei amewahimiza wakristu kusalia watulivu na kuishi vyema maisha yao kwa kuiga mfano wake padre Allois.
Wakati wa mahubiri yake askofu Lelei aliwaongoza waombolezaji katika kuimba wimbo alioupenda padre Allois kwa jina ‘Kiptaiyat Jesu”
Hii hapa sauti yake padre alloys akiimba wimbo huo katika mojawapo wa hafla za Misa.
