Shirika la watawa wa kimishonari wa Benediktini limesitisha huduma zao katika bonde la Kerio hadi pale bonde hilo litakaporejelea hali ya utulivu na Amani.
Katika waraka iliyotumwa kwa vyombo vya habari mama mkuu wa shirika hilo mtawa Rosa Pascal amesema kuwa wamechukua hatua hiyo kutokana na wahudumu wa afya wasio wazaliwa wa eneo hilo ambalo kwa sasa wanayahama eneo hilo kutokana na misukosuko na ukosefu wa usalama ambayo kwa sasa inashuhudiwa katika eneo hilo.
Mtawa Rosa Pascal amesema kuwa hatua hii inalenga kushinikiza serikali na asasi zote za usalama kuweka mikakati ya kupata suluhu la kudumu kufuatia kudorora kwa usalama katika bonde hilo na kadhalika kutwaa silaha mikononi mwa raia.
Shirika hilo limetoa wito kwa wenyeji wa bonde la kufahamu kuwa huduma ya watawa ambao wamekuwa wakihudumu katika eneo mafaao ya wenyeji hao kwa hivyo ipo haja ya wenyeji hao kutafakari hilo.
Hata hivyo askofu wa jimbo katoliki la Eldoret kwa upande mwingine amekariri kuwa kanisa halitasitisha huduma zake katika eneo hilo na kwamba shughuli za uinjilishaji zitaendelea licha ya utovu wa usalama katika eneo hilo.
