Serikali I mbioni kupunguza zaidi bei ya unga

Bodi ya kitaifa ya nafaka na mazao nchini (NCPB) imeanza kutoa mahindi kwa bei iliyopunguzwa kwa wasagaji wa unga katika mpango wa serikali wa kudhibiti bei ya unga wa mahindi nchini.

Kwenye mahojianao ya kipekee ofisini mwake, meneja wa NCPB tawi la kaskazini mwa bonde la ufa Gilbert Rotich, amesema kuwa mpango huo wa serikali ya kitaifa unawawezesha wasagaji wa unga kununua mahindi hayo kwa bei ya Sh.4, 250 kwa kila gunia la kilo 90.

Aidha, Rotich amewasihi wakulima ambao wamehodhi mahindi yao kuyauza ili kuhakikisha kuwa mpango wa serikali wa kupunguza bei ya unga wa mahindi unafaulu na kuleta afueni kwa wakenya.

Ameongeza kuwa wasagaji wa unga wanaweze kununua mahindi kwa bei nafuu kutoka mabohari ya NCPB hapa jijini Eldoret na pia eneo la Moisbridge. Ni hapo jana ambapo wizara ya kilimo ilitangaza kutolewa kwa shehena ya kwanza ya magunia 200,000 ya mahindi kwa bodi za kitaifa za nafaka na mazao nchini ili kuuzia wasagaji wa unga wa kibinafsi pamoja na walio kwenye miungano kama njia ya kudhibiti bei ya unga wa mahindi nchini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *