Wabenediktini; Huduma yetu ni kwa faida yenu Msituue

Shirika la watawa la kimishonari wa Benediktini wanaohudumu eneo la bonde la Kerio, limeelezea kusikitishwa kwake na mauaji ya Padre Allois Cheruiyot Bett wa jimbo Katoliki la Eldoret na watu wasiojulikana wiki iliyopita katika kaunti ya Elgeiyo Marakwet.

Akisoma rambi rambi kwa niaba ya watawa hao wakati wa Misa ya wafu katika Kathedrali ya Moyo Mtakatifu wa Yesu hapa jijini Eldoret, Mama mkuu wa shirika hilo hapa nchini Sr. Rosa Paschal, amesema mauaji hayo ni ishara ya kutothamini huduma za watumishi wa Mungu wanaojitolea kuisadia jamii.

Ametoa wito kwa serikali kupitia asasi zote za usalama kukomesha visa vya utovu wa usalama na mauaji vinavyoendelea kushuhudiwa katika eneo la bonde la Kerio.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *