Wakazi wa kaunti ya Uasin Gishu ambao wamekuwa wakipinga vikali hatua ya kampuni ya maji na usafi ya ELDOWAS kuongeza ada ya huduma za maji kwa asilimia 300, wamewasilisha lalama zao mahakamani.
Wakazi hao wakiwemo wanaharakati na viongozi wa mashirika mbalimbali, walitia saini hoja ya kupinga hatua hiyo na hata kuchanga fedha za kuwalipa mawakili.
Wanaratibu kufika katika mahakama kuu ya Eldoret kuwasilisha kesi hiyo ambayo wameitaka kuskilizwa kwa dharura.
Wakazi hao wanaowakilishwa na wakili Mathai Maina na Karira Nabasenge, wanadai kuwa hawakuhusishwa wala kushauriwa kuhusu mpango wa kutaka kuongeza ada za maji na kwamba wameshangazwa na hatua hiyo ya kampuni ya ELDOWAS, kwani wengi wa wakazi hawatamudu gharama ya maji.
Kesi hiyo inatarajiwa kuskizwa hii leo mbele ya jaji Reuben Nyakundi.