wizara ya afya nchini imewataka wakenya kupuuza madai kwamba chanjo inayotolewa ya polio si salama ikisema kwamba chanjo hiyo imechunguzwa na kudhibitishwa kuwa bora.
katibu katika wizara ya afya ya Umma Mary Muthoni alipuuza madai hayo ambayo imewafanya baadhi ya wazazi kuwa na wazo la kutoruhusu wanao waliochini ya umri wa miaka mitano kupewa chanjo hio.
Muthoni alisema kwamba,shirika la Afya Duniani WHO ilichunguza na kudhibitisha chanjo ya Polio akiongeza kwamba,serikali haiwezi kutoa chanjo ya aina yoyote ambayo kwa njia moja au nyingine huenda ikaathiri afya ya watu wake.
Kampeni ya serikali ya kutoa chanjo ya polio ilimalizika ambapo watoto milioni 3.6 kati ya milioni 4.2 waliolengwa wakipokea chanjo hiyo inawakilisha asilimia 86 ya walengwa huku akipuuza madai kuwa chanjo hiyo si salama kwa watoto.
Wakati uo huo kamati ya kitaifa ya ushauri wa usalama wa chanjo imeyakosoa baadhi ya makundi ya kimataifa kwa kile wanachosema ni jaribio la kuzuia kampeni hiyo ya chanjo.