ASKOFU SUBIRA:Acheni siasa

Huku shughuli za kumngatua mamlakani kama naibu Rais Rigathi Gachagua kutokana na kile inaaminika kwamba kukiuka sheria,wito umetolewa kwa Wakenya kuendelea kuliombea taifa ili kila mmoja aweze kuishi kwa amani.

Kwa mujibu wa askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nairobi Philip Anyolo Subira,taifa la Kenya ni kubwa kuliko kila mmoja yule na hivyo haja ya uwiano na utangamano.

Hata hivyo,askofu Anyolo alisisitiza haja ya viongozi wa kisiasa kumakinikia matamshi yao isije ikawagonganisha Wakenya na hili anasema itachangia kuzorota kwa amani iliyopo nchini.

Wakati huo,askofu mkuu Anyolo aliwataka viongozi waliochaguliwa kuwajibikia utendakazi wao kwa manufaa ya maendeleo ya nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *