Baraza la makanisa nchini NCCK limewapongeza vijana Kwa kujitolea kwao kueneza neno la amani kabla ,wakati na hata baada ya uchaguzi mkuu ulipita na kujihusisha na maswala ya kimaendeleo.
Kulingana na mwakilishi wa vijana katika Baraza hilo ukanda wa North Rift Samwel Sholei akiongea wakati wa kongamano la vijana kutoka ukanda huo ni kuwa,lengo kuu lilikuwa kuendelea kuwahamasisha vijana kujitenga na makundi yasiyofaa na kupokea mbinu mwafaka za kujiimarisha na kupata pesa.
Amesema kwamba kongamano hilo vilevile likwashauri vijana kuendelea kuwa mabalozi wa amani huku akishauri Serikali za kaunti ya kitaifa kuhakikisha Kila muda inawahusisha vijana katika maamuzi yake.
Kongamano hilo liliwavutia vijana kutoka kaunti za Turkana, Trans Nzoia, Nandi, Pokot Magharibi, Uasin Gishu, na Egeyo Marakwet.