Maonyesho ya kilimo ya Eldoret yakiingia siku ya pili ,wito umetolewa kwa wakulima kutoka maeneo mbalimbali wajitokeze waweze kukutana na wataalam wa kilimo na waweze kuongeza maarifa yao zaidi kuhusu kilimo na uzalishaji zaidi wa mazao yao.
Akiongea katika ukumbi wa maonyesho hayo viungani mwa mji wa Eldoret,naibu mwenyekiti wa maonyesho ya kilimo ya Eldoret Silas Maiyo amewapa motisha wakulima kutumia fursa ya upatikanaji ya wataalam kuongeza pato lao na waweze sio kujikimu tu kwao kimaisha hata kusadia katika kuongeza kapu la chakula nchini.
Kauli ambayo iliungwa mkono na mbunge wa Kesses Katika Kaunti ya Uasin Gishu Julius Ruto ambaye aliwataka wakulima katika eneo bunge lake kuwa mstari wa mbele kufika katika maonyesho hayo wajifunze na kutumia mfumo wa teknolojia ya kisasa kwenye kilimo chao.