Wito umetolewa kwa maklero kuwa mashuhuda wa kristu kwa kuonyesha mfano mwema wanapotenda kazi katika shamba la bwana.
Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nairobi Philip Anyolo akihubiri katika misa ilyowaleta pamoja makleri, watawa na majandokasisi, kama sehemu ya maadhimisho ya Sikuu ya Kutolewa Bwana Hekaluni, askofu mkuu Anyolo ametoa wito kwa viongozi wa Kanisa kuwa ni kielelezo cha huduma na mashuhuda wa upendo.
Aliwataka wote kujenga utamaduni wa maisha ya sala, kushinda kishawishi cha kumezwa na malimwengu, wazamishe maisha katika neno la Mungu, Sakramenti, Mafundisho tanzu na ushuhuda amini kwa Kanisa na Ulimwengu katika ujumla wake.
Askofu mkuu aliwataka makleri hao kuweka kanisa katika ramani na kuelimisha jamii, akisema kuwa kanisa la sasa linakumbana na changamoto si haba, changamoto hizo zikiitaji utatuzi kutoka kwa kanisa.