Wakaazi Eldoret kunufaika na nyumba kwa bei nafuu

Serikali ya kitaifa kwa ushirikiano na ile ya kaunti hii ya Uasin Gishu imeweka mikakati ya kuona kuwa inatimiza ajenda ya kuwapa wakenya makaazi ilivyohaidi kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka uliopita.

Katika mkao uliowaleta pamoja waziri wa ardhi Zakaria Mwangi Njeru na gavana wa kaunti hii ya uasin gishu Jonathan Bii Chelilim katika ziara yake kwenye kaunti hii, waziri huyo amesema kuwa tayari wametambau ardhi ya ekari elfu moja kwenye kaunti hii, ambapo wanatarajia kuanza ujenzi wa makaazi hayo, akidokeza kuwa kuanzia juma lijalo serikali ya kitaifa itatangaza maeneo hayo ili kuwavutia wawekezaji ambao watanunua kwa ajili ya mpango huo.

Waziri huyo kadhalika alihaidi kuwa hivi karibuni watatoa hatimiliki kwa wakaazi wa kaunti hii ambao wanamiliki ardhi zao kihalali ilhali hawana vyeti hivyo.

Naye gavana Jonathan Bii alisema kuwa serikali yake kwa ushirikiano na ile ya kitaifa itahakikisha kuwa hatimiliki hizo zinapatikana haraka iwezekanavyo, akitoa wito wakaazi ho kuwa na subira wanaposhughulikia swala hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *