CCIO KIMULWO:Kuna usalama wa kutosha msimu wa sikukuu

Afisa msimamizi wa uchunguzi wa jinai CCIO katika kaunti ya Uasin Gishu Peter Kimulwo ameweka bayana kwamba hali ya usalama imeimarishwa msimu wa krismasi unapokaribia.


Akionogea afisini mwake mjini Eldoret alisema maafisa wa usalama watashika doria kila mtaa na kila eneo kuwahakikishia wenyeji usalama wao hivyo akiwataka wakaazi kutohofu lolote maana amesema mali yao iko salama.


Vilevile Kimulwo alisema kuwa kuna maafisa wa kutosha kutoa usalama kwani amedokeza kwamba maafisa wote waliokuwa kwenye likizo wamerejea kazini.

Wakati huo alisema kuwa wamefanya makubaliano na wamiliki wa mihakawa na vilabu kufungwa kwa maeneo hayo ifikapo muda wa saa tano usiku ndipo wateja wao wasije wakawa waathiriwa ambao wezi watawapora wanaoelekea manyumbani mwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *