Vijana nchini wamehimizwa kutumia ujana wao kulieneza neno lake kristu na kumkaribisha huyo yesu maishani mwao ndipo wawekwe salama katika kuuridhi ufalme wa mbingu.
Akiongea wakati wa sherehe ya Family day ya Central Denary katika kanisa la Mtakatifu Maria Msongari askofu mkuu wa Jimbo kuu Katoliki la Nairobi Philip Anyolo amewataka vijana hao kuongozwa na mafundisho yake kristu kwa kujitenga na mambo yasiyostahili katika maisha ya ukristu na kuwaelekeza wengine.
Askofu vilevile aliwahimiza vijana hao kuelewa kwamba kupitia changamoto ambazo wanazipitia ndio inaweweka kusimama imara katika mafundisho yake kristu.
Aidha,askofu aliwataka wakristu na viongozi wa kanisa kuwaelekeza vijana kwa kuwashika mkono wanapopitia changamoto katika maisha kwa anachosema ni watu wa kukata tamaa kwa haraka.