Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich ameiomba serikali ya kitaifa kuyanunua mahindi ya wakulima wa humu nchini kabla ya kuzingatia wazo la kuagiza mahindi kutoka mataifa za nje.
Akiongea mjini Eldoret,Kimengich alisema kwamba wakulima nchini wanayo mahindi ya kutosha na itakua jambo la kusikitisha iwapo watasalia na mazao yao iwapo serikali haitawanunulia mahindi hayo.
Askofu vilevile aliishauri serikali kuhakikisha imefanya utafiti wa kutosha kuhusiana na vyakula vya kuzalishwa kwa njia ya kisaki GMOs kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kuyanunua au kuagiza ama hata kuzalisha vyakula kwa mfumo huo.