JAMAL:Maisha yangu hatarini

Kiongozi wa muungano wa vijana ya Youth Daawa kanda la kaskazini mwa bonde la Ufa Jamal Diriwo Omar anasema anahofia maisha yake baada ya kutishiwa maisha na baadhi ya maafisa wa usalama kwa kusimama kidete kutokana na utata wa mali yanayomilikiwa na muungano huo wa waislamu ambayo ingali inasikizwa mahakamani.

Akiongea mjini Eldoret Jamal alisema kwamba ametishiwa maisha mara si moja na mnamo Januari 21 mwaka huu alipiga repoti kwenye kituo cha polisi mjini Eldoret na licha ya kufanya hivyo hakuna hatua yoyote imechukuliwa.

Kiongozi huyo anadai  haki yake akisema imemwathiri mno kikazi na hata kuhofia familia yake kuwekwa kwenye hatari.

Ikumbukwe kuwa kiongozi huyo amekua akishughulikia kesi ya kutaka mali ya muungano wa waislamu kanda la North Rift kwa umiliki wa mali ambayo ni pamoja na majumba katika mji wa Eldoret na viungani mwake kesi ambayo yapita miwaka miwili sasa ikiwa mahakamani na haijatatuliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *