baadhi ya wabunge eneo la bonde la ufa wakiongozwa na mbunge maalum wa chama cha UDA Joseph Wainaina wameapa kuwa sharti makamishna wanne wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini ya IEBC waondolewe afisini licha ya tishio za mandamano kutoka kwa mrengo wa upinzani.
Akiongea mjini Eldoret,Wainaina alisema kwamba licha ya upizani kuahirisha mandamano yaliyoratibiwa kati miji ya mikuu ya Nairobi , Nakuru , Mombasa na mji wa Kakamega hadi mwezi ujao, serikali haitaruhusu kuwepo mandamano hayo na wala bunge halitashawishika kutopitisha kubuniwa tume ya kuchunguza na kupendekeza kuondolewa makamishna hao.
Alidokeza wanne hao wakiongozwa na naibu mwenyekiti wa IEBC Juliana Cherera na wenzake ambao hawakuafikiana na mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati kuhusiana na matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 Sharti wangatuliwe.