KIGAME:NCPB nunua mahindi kwa bei ya kuridhisha

Aliyekuwa mwaniaji kiti cha urais nchini kwenye uchaguzi mkuu uliopita wa Agosti 9 mwaka huu Rueben Kigame amesikitikia hali ambayo serikali inapania kuagiza mahinid kutoka mataifa za nje kwa anachosema mahindi ingali ipo na wakulima wa humu nchini.


Akiongea mjini Eldoret wakati wa kupokea chakula cha msaada kwa waathiriwa wa baa la Njaa zitakazoelekewa katika kaskazini mwa nchi,Kigame amesema kwamba ingekuwa vyema serikali kuyachukua mahindi yaliyo kwenye maghala ya wakulima wa humu nchini kabla ya kuanza kuagiza bidhaa hiyo.

Vilevile,Kigame aliishauri usimamizi wa halmashauri ya nafaka na mazao nchini NCPB kuhakikisha imeongeza bei ya mahindi na nafaka ndipo wakulima wafurahie matokeo ya mazao yao kwani anasema walitumia muda mwingi na pesa kuzalisha mahindi kutokana na kupanda kwa gharama ya pembejeo.


Aidha,aliwataka wakenya na wahisani kuzidi kujitokeza kuwapa msaada wananchi ambao wanakabiliana na baa la njaa akisema ni janga la kitaifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *