JIANDAENI KUWA JIJI

Mwenyekiti wa manispaa ya Eldoret Julius Kitur aliwaomba wenyeji hasa wamiliki wa vyumba vya biashara mjini Eldoret kuungana mkono na uongozi wa manispaa kuafikia malengo ya Eldoret kuwa mojawapo ya jiji nchini.

Akiongea mjini Eldoret ,Kitur alisema kwamba wamekwisha andaa mkutano na baadhi ya washikadau katik sekta mbalimbali kuhusiana na jinsi ya kuelekeza juhudi zao kwenye mji wa Eldoret na hivi karibuni ataanda mkutano na wamiliki wa vyumba hivyo kuafikiana namna watapaka rangi vyumba hivyo kwa hitaji linalokubalika.

Mwenyekiti huyo kadhalika,aliweka bayana kuwa mojawapo ya maswala hitajika za kuwa jiji ni hali ya usafi na kuwaomba wakaazi kuchukua jukumu la kuliweka mji huo safi kila wakati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *