USAFI WA MJI

Serikali ya Kaunti ya Uasin Gishu imezindua wiki ya kusafisha mji wa Eldoret lengo likiwa kupambana na utupaji ovyo wa taka mjini.


Akiongea wakati wa kuzindua zoezi hilo lililowahusisha washikdadau kutoka vitengeo mbalimbali na sekta mbalimbali,naibu gavana wa kaunti ya Uasin Gishu John Barorot aliwataka wenyeji kuchukua jukumu la kuwa mabalozi wa mazingira safi ndipo makaazi yao na mji wa Eldoret iwekwe safi kila muda.

Barorot alisema kwamba serikali itaweka pipa za taka katika maeneo yote ya umma ndipo wenyeji wasiwe na ugumu wa kutupa taka.

Kwa upande wake,waziri wa mazingira na maji katika kaunti ya Uasin Gishu Abraham Serem akiwataka wenyeji kuwajibikia mazingira yao na kuyaweka safi kila muda ndipo waepukane na maradhi yanayotokana na uchafu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *