Baraza la maimamu kaskazini mwa bonde la ufa limepongeza hatua ya kupendekezwa kuondolewa kwa shule bweni kwenye shule za msingi.
Wakiongozwa na mwenyekiti wao Sheikh Abubakar Bini ni kwamba hatua hiyo imekuja kuchelewa kwani ilifaa kuondolewa kitambo kwa kuwa watoto wa shule za msingi wangali wadogo mno kuruhusiwa kulala shuleni.
Akiongea mjini Eldoret,Bini alisema kwamba hatua hii itasaidia sasa kwa wazazi na pia viongozi wa dini kupata nafasi ya kuwashirikisha watoto hao kwenye shughuli za jamii ikiwemo kupata mafunzo za dini na hata za kinyumbani.
Vielvile alisema shule za bweni zinastahili tu kwa watoto ambao wamekomaa kiakili nan i wale ambao wanaweza wakijisimamia wasipokuwa karibu na wazazi wao.
Kadhalika ,viongozi hao walibaini kwamba hatua hiyo pia itasaidia jamii kupata fursa ya kuwapa mafunzo wanao kuhusiana na tamaduni na mila za kiafrika.