Viongozi wa nadhehebu mbalimbali katika eneo la Burnt forest waliandaa ibada ya maombi kushukuru wakenya kwa kushiriki zoezi la uchaguzi na kuyapokea matokeo yake kwa amani na kuendelea kudumisha amani.
Wakiongozwa na kasisi David Rono wakanisa la kianglikana na kasisi Paul Njoroge walisema kwamba hatua ambayo wakenya walichukua hasa ikizingaitwa kwamba kumekuwa na fikira kwamba eneo la Burntforest ni miongoni mwa maeneo ambayo huenda utovu wa usalama ukashuhudiwa kutokana na watu kutoka jamii mbalimbali kuishi maeneo hayo maswala hayo hayakushuhudiwa kwa hili wakisema hatua hiyo ni nzuri.
Viongozi hao walisema ni fursa nzuri kwa wakenya sasa kuunganika kwa pamoja kusukuma ghurudumu la ujenzi wa taifa kwa kutangamana katika maeneo mbalimbali kuishi maeneo hayo jambo ambalo wanasema lilienda kinyume na fikra mbaya za watu ha wanaosema hawana nia njema kwa wenyeji wapenda amani .
Kadhalika,viongozi hao wakishauri serikali mpya iliyo mamlakani kuwapa nafasi sawa za kazi kwa wakenya wote bila ya mapendeleo yoyote wakieleza ujenzi wa taifa inapitia kuungana kwa wakenya wote.