CHABUGA:Endeleeni kudumisha amani

Askofu mkuu wa kanisa la African divine nchini John Chabuga anasisitiza haja ya utafiti wa kutosha kufanyika kuhusiana na vyakula vinavyozalishwa kupitia njia ya kisayansi ya Gmo ili kuhakikisha vitakua salama kwa matumizi ya wakenya

Chabuga aidha alitaka swala hilo lisiingizwe siasa na badala yake maoni ya washika dau wote yaweze kujumuishwa katika mipango ya serikali ya kuondoa marufuku ya ukuzaji wa vyakula kwa teknologia hiyo .

Akizungumza katika eneo la soy katika kaunti ya Uasin Gishu askofu huyo hata hivyo alisisitiza haja ya serikali kuweka mikakati ya kuangalia maslahi ya wakulima wa humu nchini hatua ambayo alisema itasaidia kuwepo kwa usalama wa chakula nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *