Serikali pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali yametakiwa kushirikiana pamoja na kanisa ili kutafuta suluhu la kudumu la kukabiliana na baa la njaa nchini.
Padre mkuu wa jimbo katoliki la Eldoret William Kosgei alisema kuwa ushirikiano huo ni njia bora ya kutatua mzozo unaoibuka wa chakula nchini, swala hilo lisipotatuliwa kwa haraka na huenda likawa janga la kitaifa.
Vile vile aliishukuru serikali kwa kuweka mikakati madhubuti na kuhakikisha kumepatikan kwa utulivu na amani katika eneo la Kerio Valley.
Alitoa wito wa hamasisho la umma kwa jamii kama njia moja ya kupiga jeki swala la usalama katika eneo hilo.