BISHOP ANYOLO:GMO ichunguzwe

Askofu mkuu wa jimbo kuu Katoliki la Nairobi Philip Anyolo, alisema utafiti unaendelezwa kubaini ikiwa vyakula vinavyokuzwa kisayansi GMO ni salama kwa matumizi wa binadamu.

Askofu Anyolo alisema ikiwa utafiti na uchunguzi wa kanisa utaonyesha kuwa vyakula hivyo si salama, basi kanisa katoliki litajitokeza waziwazi na kutoa msimamo wake.

Kauli yake inajiri kufuatia hatua ya serikali kuondoa marufuku ya uagizaji na ukuzaji wa vyakula hivyo vya GMO, suala ambalo limeibua hisia tofauti miongoni mwa wadau katika sekta ya kilimo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *