Mahakama kuu ya Eldoret imeagiza mwanafunzi mwenye umri wa miaka 14 wa gredi ya nne anayekisiwa kumuua shemeji wake wa kiume Kwa kumdunga kisu miezi mitatu iliyopita atasalia kwenye rumande ya watoto Kwa muda ya majuma matani yajayo.
Akitoa agizo hilo jaji Eric Ogola alisema Kwa sababu za usalama wa mtoto huyo inalazimu Mahakama kuchukua hatua hiyo hadi pale mazingira salama ya kuruhusiwa mwake kupewa dhamana yatakapoafikiwa.
Mtuhumiwa aaminika kuhusika na mauaji hayo akishirikiana na dada wake mkubwa Lucy Njeri mwenye umri wa miaka 27 ambao washukiwa kumdunga kutumia kisu cha jikoni marehemu kisa kilichotokea mnamo Agosti 7 mwaka huu katika mtaa wa Manyatta huko Moi’s bridge Kaunti ya Uasin Gishu .
Upande wa mashtaka ulieleza Mahakama kwamba mtoto huyo alichukua kisu cha jikoni na kumdunga mwendazake katika hali ya kuwatenganisha mshukiwa mwenza na marehemu kutokana na mzozo wa kileo na juhudi za kumokoa shemejiye zikiambulia patupu akiaga Dunia alipofikishwa kwenye hospitali ya Moi’s bridge.
Hapo awali Mahakama ilikua imeagiza washukiwa hao Wawili kufanyiwa uchunguzi wa kiakili katika hospitali ya mafunzo na rufaa moi na pia miaka kabla ya kufikishwa mahakamani.
Mahakama ikiamuru mshukiwa mdogo kusalia kwenye rumande ya watoto huku mshukiwa mwingine akipelekwa kwenye rumande ya wanawake ya Eldoret.
Kesi hiyo itatajwa mnamo Novemba 17 2022.
kesi itatajwa mnamo Novemba 17 mwaka huu.