BUNGE LATARAJI KUANZA RASMI MCHAKATO WA KUWAPIGA MSASA MAWAZIRI

Bunge la kaunti ya Uasin Gishu limesema litaanza mchakato wa kuwapiga msasa mawaziri walioteuliwa kaunti ya Uasin Gishu.


Kulingana na spika wa bunge hilo Philip Muige ni kwamba zoezi hilo litang’oa nanga rasmi jumatatu juma lijalo hadi jumatano wakati mawaziri kumi walioteuliwa na gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Jonathan Bii Chelilim wakipigwa msasa.

Wakati huo aliwashauri wawakilishi wadi kujisatiti kutimiza matakwa ya wenyeji akieleza kwamba atashirikiana nao ili kufanikisha ndoto za wakaazi ya kupata maendeleo.

Kadhalika aliwataka wenyeji katika kaunti ya Uasin Gishu kuwa na subra na viongozi wao Kwa kuwaunga mkono kutimiza maswala hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *