MAHAKAMANI:Lomorukai matatani

Gavana wa kaunti ya Turkana Jeremiah Lomorukai anatarajiwa kufika mbele ya mahakama kuu ya Eldoret mbele ya jaji  Reuben Nyakundi mnamo Novemba  7  kuhusiana na tuhuma za kughushi stakabadhi za masomo.

Gavana huyo alilizamika kufika mahakamani kutafuta usaidizi baada ya kutaarifiwa kuwa mali yake yalikuwa yaazuiliwe na maafisa wa kupambana na ufisadi nchini EACC ambapo alipewa dhamana ya 20,000 na Mahakama hiyo.


Lomorukai atafunguliwa mashtaka matatu ikiwemo kughushi stakabadhi,kutoa taarifa isiyokuwa sahihi kwa tume ya kupambana na ufisadi na kutoa stakabadhi ghushi kinyume na sheria ya nchi ibara ya 353 ya kanunu ya adhabu.


Akiongea na wanahabari mjini Eldoret meneja wa tume ya EACC kanda la Kaskazini mwa bonde ufa EACC Japhet Baithalu alisema kama tume haina nia yoyote ya kumkamata gavana huyo kwa sababu mahakama imekwisha mpa dhamana.


alisema kwamba walifahamu kwamba gavana huyo alighushi stakabadhi zake baada ya aliyekuwa waziri wa kaunti hiyo wa miundombinu,barabara na ujenzi wa umma Benson Lokwang kuweka wazi madai ya cheti cha kughushi cha kitaaluma.


kulingana na afisa mkurugenzi wa EACC nchini  Twalib Mbarak alisema gavana huyo wa  Turkana yuko miongoni mwa viongozi 241 ambao tume hiyo inawachunguza kuhusiana na sakata mbalimbali.


Aliongeza kwamba gavana huyo alijipoatia cheti cha shahada na kile cha diploma kuchikatia tiketi cha kuwania kiti hicho cha ugavana kwenye uchaguzi mkuu uliopita wa Agosti 9 mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *