MURYUKI:Tupo tayari kwa cbc

Mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Uasin Gishu Harrison Muryuki amesema wizara hiyo iko tayari kuwapokea wanafunzi wa shule za upili ngazi ya kwanza chini ya mtaala wa umilisi wa CBC.


Akiongea afisini mwake mjini Eldoret alisema asilimia tisini na nne ya ujenzi wa madarasa yamekamilika na shule zote za umma zitawapokea wanafunzi wa junior secondary ifikapo mwaka ujao.
Afisa huyo alieleza kuwa wamewapa mafunzo walimu zaidi ya 1000 kuhusu mtaala huo.

 Alizihimiza shule za kibinafsi vilevile kupokea CBC akieleza kuna shule za kibinafsi yapatayo 500 katika kaunti nzima ya Uasin Gishu ila kati ya shule hizo 150 pekee imeafikia mfumo huo.

Hata hivyo,afisa Muryuki aliwataka wazazi ambao wanao watajiunga na shule za upili kitengo cha kwanza kufika shuleni kupata maelezo ya jinsi ya kusajili wanao kupata shule ambazo watajiunga nazo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *