GAVANA CHELILIM:Afya bora

Gavana wa kaunti ya Uasin Gishu  Jonathan Bii Chelilim alitoa hakikisho kuwa kuna madawa ya kutosha kwenye kituo cha kuhifadhi madawa hayo.

Akiongea katika hospitali ya wilaya ya kaunti ya Uasin Gishu,Chelilim aliwahakikishia wenyeji kukarabatiwa kwa majengo zee kwenye hospitali hiyo na kuimarihwa kwa hudumu za afya kwenye kituo hicho.

Chelilim vilevile alisema kuwa serikali yake itahakikisha maswala yote ya kimsingi kwa wahudumu wote wa afya katika kaunti yamehangaziw kwa huduma bora kwa wenyeji.

Kadhalika ,gavana huyo alisema watahakikisha kwamba huduma zote zimerekodiwa kwa njia ya kidijitali kwa huduma bora nay a haraka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *