Shule ya msingi ya our lady of assumption Majengo iliaandaa tamasha ya nyimbo ,kama njia moja ya kukuza talanta miongoni mwa wanafunzi, ikiwa ni mojawapo ya hitaji la mtaala mpya wa umilisi CBC.
Tamasha hiyo ikiandaliwa na wanafunzi wa gredi ya tatu, kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni uzalendo, wanafunzi wakiimba nyimbo za kusifu taifa hili, pamoja na nyimbo za kishujaa kama njia moja ya kuwafahamisha wanafunzi maswala yanayohusu sifa za taifa hili.
kulingana na Bramuel Kuloba ni mwalimu wa gredi ya tatu wanafunzi hao wametia fora kwenye talanta zao na wataendelea kukuza talanta hizo shuleni huku akiwaomba wazazi kuwasaidia wanao kutambua talanta zao.
Shule hiyo ya our lady of assumption Majengo inayodhaminiwa na kanisa katoliki jimboni, ni mojawapo ya shule ambazo zimekuwa zikitia fora zaidi katika mitihani ya kitaifa.
Haya yanajiri huku serikali kupitia wizara ya elimu, ikiongeza muda wa siku kumi zaidi, kwa wanafunzi wa gredi ya sita ili kuchagua shule ambazo watajiunga nazo kutokana na hitaji la mtaala mpya wa CBC.
Waziri wa elimu profesa George Magoha akikagua ujenzi wa madarasa ya mtaala huo, alidokeza kuwa wazazi sasa wana muda wa siku kumi zaidi kufanya hivyo.
Magoha kadhalika alitoa onyo kwa walimu wanowafukuza wanafunzi shuleni kwa kutokamilisha karo, akisema kuwa ni kinyume cha sheria, na walimu hao wanafaa kuafikiana na wazazi ili kukubaliana jinsi ya kukamilisha karo.