BISHOP KIMENGICH:mpokee matokeo kwa ujasiri

Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich ametoa wito kwa viongozi wakuu wawili, ikiwa ni rais mteule William Ruto na kinara wa azimio la umoja Raila Odinga kuwa tayari kukubali maamuzi yatakayotolewa na mahakama ya upeo kuhusiana uchaguzi mkuu katika wadhifa wa urais.

Vikao vya kusikizwa kwa kesi hiyo katika mahakama ya upeo  vikianza rasmi juma hili, askofu Kimengich alimpongeza kinara wa azimio la umoja one Kenya Raila Odinga, kwa kufuata taratibu za kisheria za kuelekea mahakamani kutafuta haki, akiwataka Raila na rais mteule William Ruto kuwatuliza wafuasi wao, haswa katika kipindi cha kusikizwa kwa kesi na maamuzi ya kesi hiyo mahakamani.

Askofu Kimengich kadhalika alitoa wito kwa wakenya na viongozi nchini, kukumbatia maridhiano baada ya uchaguzi mkuu kwa faida ya mshikamano wa kitaifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *