WA DINI:Uchaguzi wa amani

Viongozi wa kidini katika kaunti ya Uasin Gishu wamewataka wakaazi katika kaunti hiyo kuhakikisha wameimarisha amani kabla ,wakati na hata baada ya uchanguzi mkuu wa Agosti tisa mwaka huu na kukoma kutumia vileo ambayo wanasema inawasababisha kuzua rabsha.


Wakiongozwa na mwakilishi wao kanda la kaskazini mwa bonde la ufa kasisi George Gichana wa kanisa la Deliverance church Eldoret wakizungumza mjini Eldoret waliwataka vijana kujiepusha kubugia pombe ambayo walisema linachangia pakubwa sana wao kujihusisha na rabsha.

Hata hivyo,viongozi hao walipendekeza serikali kuu kutoa amri ya kufungwa kwa maeneo ya burudani siku moja kabla ya uchaguzi hadi uchaguzi huo ukamilika kwa hili wakieleza huenda wanasiasa ambao wanayo hulka mbaya ya kuwanunulia pombe vijana kuzua rabsha wakakabiliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *