Maafisa wa polisi wamemtia mbaroni mwanamume mmoja anayeshukiwa kumuuwa jirani wake katika kjiji cha Cheptobot eneo bunge la Marakwet Magharibi , Kaunti ya Elgeyo Mrakwet.
Polisi wanasema walifanikiwa kumpata jamaa huyo kwa jina Evans Kipchirchir baada ya kutoroka kifuatia kifo cha jirani wake
Mkuu wa polisi katika eneo hilo John Matasi amesema bado wanawasaka washukiwa wengine tano ambao walishirikiana kumuua jirani wao kufuatia mzozo wa ardhi. Matasi aidha ameongeza kuwa washukiwa wengine wanaaminika kutorokea Kaunti ndogo ya Marakwet mashariki, huku akiwataka walio na ripoti kuhusiana na kisa hicho kuripoti kwa ofisi husika.
