muungano wa wahudumu wa bodaboda nchini sasa unalenga kusajilisha wahudumu zaidi ya millioni 1.3 kote nchini katika juhudi za kuweza kuwatambua kwa urahisi pindi kunapokuwa na tatizo. mwenyekiti wa muungano huo nchini kevin mbadi amesema wahudumu wengi wamelaumiwa kufuatia kudorora kwa usalama katika maeneo mbalimbali nchini jambo ambalo anasema litafika kikomo kupitia mpango huo