Jamii ya Wafugaji kufunzwa kupata mapato kupitia Shanga

Serikali kupitia mradi wa ushanga initiative inalenga kuwapa mafunzo  kina mama kutoka jamii za wafugaji  kuhusu  jinsi  ya kutumia shanga kutengeneza  bidhaa zitakazowapa pesa ili kuwasaidia kujikimu.

 Mradi huo unalenga kutoa mafunzo  kwa akina mama kutoka kaunti saba ikiwemo pokoti magharibi  huku akina mama  150 wakisajiliwa kutoka kwa kila kaunti ndogo.

 Katibu katika wizara ya michezo na utamaduni  Josphedha Mukhobe anasema kuwa  mradi huo unalenga kuwawezesha kina mama  kujitegemea kupitia njia ya  kitamaduni  ikiwemo kutengeneza bidhaa kupitia shanga.

Gavana wa kaunti hiyo john lonyangapuo amesifia  hatua hiyo kama njia mwafaka ya   kuimarisha uchumi eneo hilo na kuwainua kina mama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *