Ipo haja ya kujenga vyuo vya serikali vya kutoa mafunzo na sheria katika miji mbalimbali nchini. Akifika mbele ya kamati ya seneti kuhusu haki na sheria kuelezea kuhusu taaluma hii, aliyekuwa mwanasheria mkuu chini Prof Githi Muigai amesema ilivyo kwa sasa wanafunzi wengi maeneo mbalimbali nchini wanapitia hali ngumu kusaka masomo katika chuo hicho jijini Nairobi hali ambayo pia inasababisha msomgamano katika chuo hicho.