Kiranja wa wengi katika seneti na ambaye pia ni seneta wa Murang’a Irungu Kang’ata, amejikuta pabaya baada ya kushambuliwa vikali mtandaoni aliposema wakati wa kufungua shule umewadia.
Akitoa matamshi hayo kwenye mtandao wake wa twitter Senata huyo alisema idadi ya wagonjwa wa virusi vya corona inapungua nchini na hivyo basi ni salama kwa taasisi za elimu kufunguliwa.
Wengi walihisi hakupaswa kuyatoa matamshi hayo hususan wakati huu ambapo wataalam wa afya wangali na shauku kuhusiana na hatua hiyo
Baadhi nao walionelea kuwa matamshi yalimaanisha hali ya COVID-19 nchini inadhibitiwa ikizingatiwa kuwa siku za hivi punde visa vinavyorekodiwa ni vichache.