waathiriwa wa bwawa la patel solai subukia kaunti ya nakuru wanaisihi serikali ya kitaifa kuingilia kati na kuona kwamba wanafidiwa kutokana na maafa yaliyowafika miaka miwili iliyopita.
wakiongea baada ya mkutano uliokuwa umeratibiwa na wakili wao wamesema kuwa hali ya maisha imekuwa ngumu zaidi tangu mkasa huo.
mkasa huo wa tarehe tisa mei mwaka wa 2018 ulipelekea watu 48 kufariki na mamia ya watu kuwaathirika.
mkurungenzi mkuu wa khrc george kegoro walilenga kuwafahamisha wateja wao jinsi kesi yao inavyoendelea mahakamani.