Rais Uhuru Kenyatta ameagiza bendera ya Kenya pamoja na jumuiya ya Afrika Mashariki EAC kufungwa nusu mlingoti kama heshima kwa raisa wa Burundi Piere Nkurunziza aliyefariki mapema wiki hili.
Agizo hilo sasa litafanyika katika afisi za kidiplomasia za kenya kote ulimwenguni na matekelezo yake yanatarajiwa kuanza kufanya kazi hiyo kesho Jumamosi Juni 13, mwaka huu hadi pale kiongozi huyo atakapozikwa.
Nkurunzinza alifariki akiwa na miaka 55 baada ya kudaiwa kuwa alikumbwa na mshutuko wa moyo.