Kasisi William Kapkiai kutoka kaunti ya Baringo amekashifu vikali mzozo wa hivi karibuni wa kijamii katika kaunti ya Narok ambapo,watu wawili walipoteza maisha yao kwa mapigano uliotokana na kisa cha wizi wa mifugo.
Kasisi huyo ameongeza kuwa kisa hicho cha Narok kusini inahujumu pakubwa umoja wa kijamii na kutaka viongozi wa eneohilo kuwa kwenye mstari wa mbele kuhubiri amani, hasa baada ya kubainika kuwa mzozo huo unahusiana na umiliki wa ardhi baina ya jamii mbili za eneo hilo..
Akiongea katika eneo la Tenges Kapkiai amewataka Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kutatua tofauti zao hasa wakati huu taifa ikikabiliana na janga la Korona.